Sunday, August 26, 2012

NTA 4 WAANZA MITIHANI

Wanafunzi wa masomo ya awali ya fani mbali mbali za utalii (Basic Certificate-NTA 4) .Leo wameenza rasmi mitihani yao ya kumaliza masomo leo.Habari zaidi na picha zitafuata hapo baadae

Monday, July 30, 2012

Mtaalamu kutoka PUM atembelea ZIToD

Mkurugenzi wa chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi Zuleikha .K.Khamis pamoja na walimu wa chuo wakimsikiliza mtaalamu kutoka shirika la Misaada la PUM kutoka UHOLANZI alipofika chuoni kubadilishana mawazo na wakufunzi wa chuo.

Printer Printer Printer

Mwalimu Mohd akipokea Printer kutoka kwa Mwalimu Jeury Ramadhan




ZIToD Kwenye MAI MOSI 2012 Aman-Zanzibar









Saturday, July 21, 2012

Matokeo Mbali Mbali ZIToD





Wanafunzi wa Fuoni Msingi watembelea ZIToD

 Wanafunzi kutoka skuli ya Fuoni Msingi wakifanya usafi katika maeneo ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi ikiwa ni moja ya ziara za kamati ya mazingira ya skuli hiyo
 Wanafunzi wa Fuoni Primary School  wakifanya usafi ZIToD

 Baada ya kazi za usafi wanafunzi wa Fuoni Msingi wakipata viburudishaji vilivyoandaliwa kwa ajili yao na uongozi wa chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi
Walimu waliongozana na msafara wa wanafunzi wa skuli ya msingi ya Fuoni wakipata viburudishaji.

MITIHANI YA MWISHO WA MWAKA ZIToD

Wanafunzi  wa ngazi ya Diploma wa kozi za ICT and Accounting pamoja na diploma ya uongozi katika sekta ya utalii(DHTM) wakifanya mitihani yao ya kumaliza mwaka wa masomo 2011/2012
Wanafunzi wa ICT and Account ngazi ya Diploma (NTA 6) wakifanya mitihani chuoni Maruhubi.



ZIToD WAANZA MITIHANI YAO YA MWISHO

 Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo ya Utalii na ICT kwa ngazi ya cheti ( NTA 5) wakifanya mitihani yao ya mwisho ambayo iliaza rasmi tarehe 16/07/2012.
 Wanafunzi wa kozi za FRONT OFFICE,FOOD BRODUCTION na ICT wakifanya mitihani yao katika ukumbi wa RESTAURANT
 Wanafunzi wa NTA 5 wakifanya mitihani yao ya kumalizia mwaka.
Kazi ikiendelea ya kujipima uwezo kwa wanafunzi wa ngazi ya cheti NTA 5

Friday, July 13, 2012

 Walimu wa chuo cha Maendeleo ya  Utalii  wakiwa pamoja na mkurugenzi wao Bi Zuleikha K.Khamis wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ofisi na Maktaba ya chuo.
 Jengo litakalotumika kama ofisi na maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii likionekana kwa mbele.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii wakiwa katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa jengo la ofisi na Maktaba ya chuo

 Kikundi cha sanaa ya ngoma asili kikitoa burudani kwa waliohudhuria hafla hiyo
 Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akienda kuweka jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
 Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua kitambaa kuashiria  uwekaji  rasmi wa jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
 Mheshimiwa  Mwenyekiti wa bodi ya chuo  Mh  Khamis Mussa akizungumza katika hafla ya  kuweka jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
 Mheshimiwa  waziri waq habari utalii utamaduni na michezo Mh  Said A Mbarouk akizungumza katika hafla ya  kuweka jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiongea na walimu wafanyakazi wanafunzi na walikwa waliohudhuria hafla ya  uwekaji wa  jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar.

Tuesday, July 10, 2012

UWEKAJI JIWE LA MSINGI WA OFISI NA MAKTABA YA CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR

Mh Makamo  wa pili wa rais wa Zanzibar .Balozi Seif Ali Iddi leo alijumuika na uongozi wote wa wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo pamoja  na wafanyakazi na wanafunzi  wa chuo  cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Jengo jipya la chuo litakalotumika kwa matumizi ya ofisi na Maktaba.

 Picha na habari zaidi zitapataikana hapo baadae.

Saturday, July 7, 2012

MAZOEZI YA UZIMAJI MOTO KWA WANAFUNZI WA ZIToD





Wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya Utalii  Maruhubi Zanzibar wakipata mafunzo ya kukabiliana na janga la Moto kutoka  kwa wataalamu wa kikosi cha uzimaji moto Zanzibar.Mafunzo hayo  ya  siku tano ya nadharia na vitendo yalifanyika chuoni  Maruhubi.

Tuesday, July 3, 2012

MATUKIO MBALI MBALI ZIToD

 Wanafunzi kutokaSouth Africa wakiwa pamoja na walimu wao wakipata mlo wa kienyeji wa kizanzibar(Pilau ) ambayo waliianda wao katika mafunzo  yao ya kujifunza mapishi ya Kizanzibar yaliyofanyika chuoni Maruhubi.
 Mkurugenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi Zulekha K.Khamis akitoa nasaha zake kwa wanafunzi pamoja na viongozi wa serekali ya wanafunzi iliyochaguliwa chuoni.
 Rais wa Serekali ya wanafunzi ya chuo cha Maendeleo ya Utalii (ZIToDSO)  Bw Bakar Kheri(alievaa suti na tai) akiwa na wapambe wake wakati akiingia ukumbini kwa ajili ya kula kiapo cha kuwa Rais wa ZIToDSO.
Mmoja wa wanafunzi kutioka South Afrika alieshiriki mafunzo ya siku mbili juu ya utayarishaji wa  vyakula vya Kizanzibar akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuocha Maendeleo ya Utalii Zanzibar,Bi Zuleikha K.Khamis

Wednesday, June 27, 2012

CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII (ZIToD)  KIMEFUNGUA BLOG YAKE MPYA AMBAYO MBALI NA KUTUMIA WEBSITE YAKE YA WWW.ZITOD.ORG ITAKUWA PIA INATUMIA BLOG HII KWA AJILI YA KUTOA TAARIFA NA MATUKIO MBALI MBALI YATAKAYOKUWA YANATOKEA CHUONI.
WATAKAOANGALIA BLOG HII WATAKUWA NA UWEZO WA KUTOA MAONI  YAO JUU YA KILE AMBACHO TUTAKUWA TUMEKIWEKA
AHSANTENI SANA.