Friday, July 13, 2012

 Walimu wa chuo cha Maendeleo ya  Utalii  wakiwa pamoja na mkurugenzi wao Bi Zuleikha K.Khamis wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ofisi na Maktaba ya chuo.
 Jengo litakalotumika kama ofisi na maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii likionekana kwa mbele.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii wakiwa katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa jengo la ofisi na Maktaba ya chuo

 Kikundi cha sanaa ya ngoma asili kikitoa burudani kwa waliohudhuria hafla hiyo
 Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akienda kuweka jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
 Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua kitambaa kuashiria  uwekaji  rasmi wa jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
 Mheshimiwa  Mwenyekiti wa bodi ya chuo  Mh  Khamis Mussa akizungumza katika hafla ya  kuweka jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
 Mheshimiwa  waziri waq habari utalii utamaduni na michezo Mh  Said A Mbarouk akizungumza katika hafla ya  kuweka jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiongea na walimu wafanyakazi wanafunzi na walikwa waliohudhuria hafla ya  uwekaji wa  jiwe la msingi wa jengo la afisi na Maktaba ya chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar.

No comments:

Post a Comment